Matthew 24:32-35

32 a “Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. 33 bVivyo hivyo, myaonapo mambo haya yote, mnatambua kwamba wakati u karibu, hata malangoni. 34 cAmin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia. 35 dMbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Copyright information for SwhNEN